Muigizaji nyota wa tamthilia ya Isidingo lesego Motsepe afariki

Muigizaji nyota, Lesego Motsepe, ambae alikuwa akijulikana kama Letti Matabanne katika tamthilia ya Isidingo amefariki dunia.
statement iliyotolewa kwa
niaba ya familia ya Motsepe inasema kuwa, alikutwa akiwa ameshafariki na
kaka yake "Moemise Motsepe" akiwa nyumbani kwake mida ya saa tano
asubuhi,
Mwaka
2011, siku ya ukimwi duniani, Motsepe alijitangaza hadharani hali yake
ya VVU katika kusaidia kupambana na unyanyappaa dhidi ya watu wanaoishi
na ugonjwa huo. Alifanya pia warsha
kadhaa na mazungumzo juu ya umuhimu wa kuishi kwa matumaini kwa
walioathirika na Ukimwi moja kwa moja au vinginevyo. Yeye pia alifanya
kazi kama balozi wa Ukimwi kwa miaka mingi, kuwaelimisha watoto katika
jamii mbalimbali.
Lesego
ameelezewa kama binti mwenye upendo, dada na rafiki, alikuwa ni mhitimu
wa mchezo wa kuigiza, alikuwa ni muigizaji, mshairi,na mtoa hadithi ambaye alitumia zaidi ya miaka 10 katika sehem kubwa ya tamthilia hiyo maarufu.
Motsepe
aliishi na mama yake - Ivy Skhosana na kaka zake wawili wawili -
Andile Skosana na Moemise Motsepe na wapwa mbalimbali, wajukuu, familia
yake ya kiroho na familia pana.
0 comments