Open top menu
Thursday, April 25, 2013

NATURE AKERWA NA KIPINDI CHA TELEVISHENI WAMTOA NA KUKATIZA INTERVIEW KISA KAVAA NDALA NA KAWOSH

Posted: 2013-04-20 09:21:29 UTC-07:00

Msanii mkongwe na maarufu nchini, Juma Kassin Kiroboto, aka Nature, ameonyesha kukerwa na kile kilichoendelea jana usiku katika kipindi cha burudani cha  televishen inayotizamwa africa ya mashariki alipokuwa akifanya nao interview. Nature alionekana akiwa amevaa kawosh na ndala na mara baada ya mahojiano mafupi ya mwanzo ambapo mtangazaji alisema watarejea baada ya mapumziko mafupi Nature hakuonekana tena. Kilichotokea  kwa mujibu wa Nature mwenyewe, ni wakati wa mapumziko hayo, mtangazaji wa kipindi hicho alimfata na kumuambia kuwa hataendelea na interview tena kwasababu ya mavazi aliyokuwa kavaa ambayo ni ndala na kawosh. kuonyesha kukerwa kwake na ishu hiyo Nature aliamua kuandika kupitia ukurasa wake wa facebook....
Juma Natur Kibla
hivi kwa mfano angekuwepo mzungu pale na kavaa ndala wangesitisha mahojiano na kuvaa kaoshi ni tatizo,kunywa nimekunywa bt kuna baya nimeliongea na hivi kama kweri we nimuandishi wa habari unaruhusiwa kuvaa vile kisheria kama yule mtangazaji nimeboreka kinoma na ikiwezekana nasitisha kuanzia ssa kupeleka ngoma zangu pale siitaji interview
Tagged
Different Themes
Written by Templateify

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments