-
ADAM MCHOMVU KUTAMBULISHA SINGLE 2 MPYA NDANI YA MAISHA CLUB
Posted: 2013-04-25 12:32:23 UTC-07:00
Mtangazaji wa Clouds Fm ambae pia ameamua kujiingiza katika mziki "Adam Mchomvu" A.K.A Baba Jonii, siku ya jumapili atatambulisha ngoma zake mbili mpya ndani ya Maisha Club.Siku hiyo Adam atatambulisha ngoma ambayo siku za nyuma aliwaonjesha kidooogo mashabiki wake kupitia kipindi cha XXL ikiwa kama demo, lakini kwa hivi sasa imeshakamilika "Unaakili wewe", pamoja na pini lingine alilolifanya na wasanii kutoka Rada entertainment, ambapo chini ya Rada kuna Ngwea, TID, Romy Jones na wengineo. Wasanii hao pia kutoka Rada entertainment wakuwepo kwa ajili ya kutoa perfomace, kumbuka ni jumapili hii ndani ya Maisha Club
Adam Mchomvu
ok jumapili @ club bilicanas BABA LA BABA (BABA JONII) ntazindua track zangu mbili ... ebu dondoka pale uone utofauti ya mimi na wao, ofcuz nimepika na mzee mnya ma T.i.D, ZAMBADA M2 MBAYA KAIZA SOSA BABUU WA KITAA, ROMMY JONES its rader ent baby... miss dar indian ocen watapiga show fupi.. so watu wabaya tukutane ubayani... mzee amesema!!!!!!
SONGA SOON KUTOKA NA ILLMATHEMATIX
Posted: 2013-04-25 07:58:55 UTC-07:00
Msanii wa hiphop Songa yuko mbioni kuachia pini jipya "Illmathematix" akiwa kamshirikisha Identity na One the incredible.Juma tano ijayo baada ya mapumziko ya hollyday ndefu kidogo Songa atai bless for the first time kwa radio stations kwa ajili ya kufurahisha na kufundisha akili yako.Kama hujapata kumfahamu, cheki na video ya wimbo wake "niite songa" hapo chini
SONGA
WIMBO MPYA TOKA KWA SONGA UITWAO ILLMATHEMATIX feat. IDENTITY NA ONE UTAACHIWA RASMI JUMATANO IJAYO. @fettythebest @bdozen
0 comments